Home Uncategorized YANGA WAMALIZANA NA JEMBE HILI LA KAZI, FUNDI WA KUPIGA MIPIRA ILIYOKUFA

YANGA WAMALIZANA NA JEMBE HILI LA KAZI, FUNDI WA KUPIGA MIPIRA ILIYOKUFA


BAADA ya Klabu ya Yanga kumalizana na beki wa kushoto wa Rayon Sports ya Rwanda, Eric Rutanga, uongozi wa klabu hiyo umeibuka na kudai kuwa Yanga wamepata mtu wa kazi katika eneo la ulinzi.

Mmoja wa viongozi wa Idara ya Habari na Mawasiliano ndani ya Rayon Sports, Jean Luc, alisema kuwa Rutanga ni mmoja wa wachezaji wazuri akicheza kama beki wa kushoto kwani mbali na uwezo wake wa kupanda kushambulia na kurudi kukaba, pia ana uwezo mkubwa wa kupiga faulo.
Jean Luc alisema kuwa Yanga wamepata mchezaji mzuri katika eneo la ulinzi kwa kumsajili Rutanga, kwani ni moja ya wachezaji wenye uwezo mkubwa ndiyo maana amekuwa hakosekani katika kikosi cha timu ya Taifa ya Burundi kutokana na uwezo wake.

“Rutanga ni mchezaji mzuri sana, anaweza kwenda kushambulia na akarudi kwenye nafasi yake na kusaidia kukaba, lakini ukiacha hivyo, anaweza sana kupiga mipira iliyokufa kama kona na faulo, Yanga wamepata mchezaji sahihi kusema ukweli,” alisema Jean Luc.
Meneja wa Rutanga, Harve Tra Bi alithibitisha kuwa mchezaji huyo amekubaliana mkataba wa miaka miwili wa kukipiga Jangwani. Mchezaji huyo alitumiwa mkataba kwa barua pepe kutokana na mipaka ya Rwanda kuendelea kufungwa kutokana na Corona.
SOMA NA HII  HAPA SIMBA WAVUNJE TU BENKI MAANA SIO KWA DAU HILI