Home Uncategorized AZAM FC HESABU ZAO ZIPO NAMNA HII

AZAM FC HESABU ZAO ZIPO NAMNA HII

Azam FC ipo nafasi ya tatu Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 66.

Kuhusu kushuka nafasi ya pili kwa sasa uongozi wa Azam FC umesema kuwa upo mikononi mwa Yanga ambao ndio wapo nafasi ya pili.

Ikiwa imecheza mechi 36 imeshinda mechi 19, sare 9 na kupoteza nane. Safu ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao 49 na kuruhusu kufungwa mabao 24.

Kesho, Julai 23 inakutana na Mbeya City iliyo nafasi ya 13 na pointi 42 haina uhakika wa kubaki ndani ya Ligi.

Zakaria Thabit,  Ofisa Habari wa Azam FC amesema:”Nafasi ya pili kwa sasa sisi sio waamuzi kwa kuwa Yanga ipo nafasi hiyo na ina mechi mbili mkononi ikitokea wakipoteza sisi tukashinda basi tutakuwa nafasi ya pili.”

SOMA NA HII  KIUNGO MPYA SIMBA AKOMBA MILIONI 138