Home Uncategorized BAADA YA KUBEBA KOMBE..DILUNGA AMEFUNGUKA HAYA SIMBA..!!

BAADA YA KUBEBA KOMBE..DILUNGA AMEFUNGUKA HAYA SIMBA..!!

KIUNGO mshambuliaji wa  Simba, Hassan Dilunga, amewaomba mashabiki wao kuifuata timu popote itakapokabidhiwa Kombe la Ligi Kuu Tanzania Bara.

Simba wamefanikiwa kutetea ubingwa wao kwa mara ya tatu mfululizo wakiwa bado wana michezo sita mkononi baada ya  juzi kutoka suluhu na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya.

Akizungumza  jana kupitia mtandao wa kijamii wa Klabu ya  Simba,  Dilunga alisema amefurahi  kuwa mabingwa kwa mara nyingine.

Dilunga alisema  pamoja na kutwaa ubingwa wa msimu huu, hawajui wapo watakabidhiwa  kombe hilo,  hivyo kuwaomba mashabiki kuifuata timu popote itakapokabidhiwa.

Alisema wataendelea kutwaa ubingwa kwa misimu ijayo mfululizo ili waweze kuiwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Tunafuraha sana na tunaahidi kuendelea kuchukua kombe mfululizo,”alisema Dilunga.

Simba wamefanikiwa kutetea taji hilo, baada ya kufikisha pointi 79, ambazo hazitafikiwa na timu nyingine zinazoshiriki ligi hiyo.

SOMA NA HII  SIMBA YAITUMIA BIASHARA UNITED UJUMBE HUU