Home Uncategorized FEI TOTO AKABIDHIWA TUZO YA KUWA MCHEZAJI BORA KWA MSIMU NA SportPesa

FEI TOTO AKABIDHIWA TUZO YA KUWA MCHEZAJI BORA KWA MSIMU NA SportPesa

KAMPUNI ya michezo na burudani ambao pia ni wadhamini wakuu wa timu za Simba na Yanga,SportPesa wiki hii waliendesha shindano la kumpata mchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa timu wanazozidhamini.
Kwa upande wa Yanga mshindi aliibuka Feisal Salum na kwa upande wa Simba mshindi aliibuka Clatous Chama.
Shindano hili liliwataka mashabiki wa timu hizi mbili kumpigia kura mchezaji wao bora na aliyefanya vizuri kuanzia mwanzo wa ligi mpaka hitimisho kupitia mtandao wa kijamii ambapo mshindi atakabidhiwa tunzo kama ishara ya ushindi na fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 1.
Akizungumza wakati wa kukabidhiwa tuzo Feitoto alisema,  “Kwanza kabisa napenda kuwashukuru sana wadhamini wetu SportPesa kwa kutukumbuka sisi wachezaji na kutambua zaidi vipaji vyetu kwani hii inatupa motisha ya kufanya vizuri zaidi na zaidi.
“Pili niwashukuru mashabiki wa Young Africans kwa kunipigia kura kwa wingi na kuhakikisha naibuka mshindi kwa timu yangu.  Pia napenda kuushukuru uongozi mzima wa Yanga kwa nafasi waliyonipa,kuniamini kama mchezaji wao,” alisema mchezaji soka huyo.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa, Tarimba Abbas, wakati wa mkutano na waandishi wa habari maalum kwa kukabidhi tuzo hiyo alisema, “Safari hii tumewapa nafasi wachezaji waweze kupendekeza na kumwezesha mchezaji wa timu yao pendwa kushinda kwa kumpigia kura mara nyingi wawezavyo ili kushinda zawadi hizi.
“Hii ni mara ya kwanza kwa SportPesa kutoa tunzo hizi kwa mchezaji wao bora ikiwa na lengo la kuwahamasisha na kuongeza ushindani mkubwa baina yao ambao utapelekea kwa timu nzima kuendelea kufanya vizuri zaidi na zaidi kwenye michuano ijayo.
“Nawashukuru sana mashabiki wa timu zote mbili kwa kuonyesha ushirikiano mkubwa hasa kuhakikisha wanawapigia kwa wingi wachezaji wao hadi kuibuka washindi.
Naye Msemaji na Mhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz, alimaliza kwa kusema “Msimu huu haukuwa mzuri kwetu lakini ningependa kuwaomba mashabiki waendelee kutuonyesha ushirikiano na waendelee kutamba kwani yajayo yanafurahisha.”

SOMA NA HII  CHELSEA WAIPOTEZA INTER MILAN KWA KANTE