Home Uncategorized HIYO VITA YA MTIBWA SUGAR V YANGA NI BALAA

HIYO VITA YA MTIBWA SUGAR V YANGA NI BALAA

KIKOSI cha Yanga kimeendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiweka sawa kuelekea Kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Julai 22, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro na unatarajiwa kuwa na ushindani

mkubwa ndani ya uwanja.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Luc Eymael raia wa Ubelgiji inapambana kubaki nafasi ya pili na mshindani wake mkubwa ni Azam FC. 

Yanga ina pointi 68 ikiwa nafasi ya pili huku Azam FC ikiwa nafasi ya tatu na pointi 66  zote zimecheza mechi 36.

Mtibwa Sugar inayonolewa na mzawa Zuber Katwila ina hasira ya kunyooshwa bao 1-0 mbele ya KMC hivyo inahaha kupambania nafasi ya kubaki ndani ya ligi.

Ikiwa nafasi ya 14 na pointi zake 41 haitakuwa salama iwapo itapoteza mchezo huo kisha Lipuli akapata ushindi mbele ya Ruvu Shooting atamshusha jumlajumla.

Lipuli nao pia wana pointi 41 wakiwa nafasi ya 15 mwendo wao ni wakusuasua wakiwa wamecheza jumla ya mechi 36.

SOMA NA HII  MKUDE ATOA NENO NDANI YA SIMBA, STRAIKA YANGA ATUMIKA KUTAPELI, NI KESHO CHAMPIONI IJUMAA