Home Uncategorized KILICHO NYUMA YA UWEZO WA KIPA NAMBA TATU WA YANGA HIKI HAPA

KILICHO NYUMA YA UWEZO WA KIPA NAMBA TATU WA YANGA HIKI HAPA


KIPA namba tatu wa Yanga, Ramadhan Kabwili amesema kuwa siri kubwa ya uwezo wake ndani ya uwanja inabebwa na juhudi pamoja na kujituma kwenye mazoezi.

Msimu wa 2019/20 amekaa langoni ndani ya dakika 90 na kufungwa bao moja kwenye sare ya 1-1 mbele ya Mtibwa Sugar, jana Julai 22.

Aliweza kuonyesha kipaji chake kwa kuokoa michomo miwili ya hatari ya moja kwa moja jambo ambalo limemfanya ghafla awe gumzo kwa mashabiki pamoja na wadau wa masuala ya michezo.

Hana nafasi ndani ya kikosi cha Yanga kutokana na uwepo wa makipa wawili ambao ni Metacha Mnata na Faroukh Shikhalo ambao hawa wanagombania namba moja kikosini hapo.

Kabwili amesema:”Sababu kubwa ya mimi kufanya  vizuri katika kazi yangu ni kutimiza majukumu yangu pamoja na juhudi ambazo ninazo mazoezini.

“Ushirikiano ninaoupata kwa wachezaji wenzangu nao pia unachangia kunifanya niwe hapa, bado nitazidi kupambana ili kuwa bora.”

Yanga ipo nafasi ya pili kwenye ligi ikiwa imecheza mechi 37 imebakiwa na mchezo mmoja kukamilisha mzunguko wa pili.  

SOMA NA HII  MO SALAH NA SAMATTA KUWATAZAMA WABABE HAWA WALIOTINGA ROBO FAINALI