Home Uncategorized MANCHESTER UNITED WAMALIZA TOP 4,KUCHEZA LIGI YA MABINGWA ULAYA

MANCHESTER UNITED WAMALIZA TOP 4,KUCHEZA LIGI YA MABINGWA ULAYA

MANCHESTER United iliyo chini ya Kocha Mkuu, Ole Gunner Solskjaer imehitimisha msimu wa 2019/20 ikiwa ndani ya top 4 ikiwa na uhakika wa kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Bruno Fernandes alianza kupachika bao la kuongoza dakika ya 71 kwa penalti kisha Jesse Lingard bao la pili dakika ya 90+6 wakati wakishinda mabao 2-0 mbele ya Leicester City. 

Leicester City walimaliza wakiwa pungufu baada ya Jonny Evans kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 90+4.

Ushindi huo unaifanya Manchester United kumaliza ikiwa nafasi ya tatu ikiwa na pointi 66 huku Leicester City ikiwa nafasi ya tano na pointi 62.

SOMA NA HII  SVEN HATA HAELEWI HATMA YAKE NDANI YA SIMBA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here