KAMATI ya nidhamu ya Shrikisho la Soka Tanzania,(TFF) imetoa onyo kali kwa Uwanja wa Sokoine, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya na klabu zote zinazotumia uwanja wa Sokoine kama uwanja wa nyumbani kwa kosa la mashabiki kuingia uwanjani baada ya mchezo kumalizika.
Taarifa iliyotolewa leo kupitia Ukurasa rasmi wa Instagram wa TFF imeeleza kuwa kamati inawataka Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya, wamiliki wa uwanja wa Sokoine na klabu zote zinazotumia uwanja wa Sokoine kuhakikisha zinazingatia kanuni ya 14(10), 14(11),14(42) na 14(43) inayohusu taratibu za mchezo inayosema:-
“Ni marufuku kwa viongozi kuingia uwanjani(pitch) bila sababu za msingi kinyume na taratibu za mchezo kabla, wakati au baada ya mchezo.
“Ni marufuku kwa mashabiki kuingia uwanjani kabla,wakati au baada ya mchezo.Katika mchezo wowote wa ligi kuu wakati mchezo ukiwa unachezwa hairuhusiwi kufanyika shughuli nyingine yoyote katika uwanja wa kuchezea na eneo la uwanja wa ndani ya uzio wa ndani wa uwanja kama vile muziki, ujenzi na kuendeshwa kwa vyombo vya moto na visivyo vya moto.
“Hairuhusiwi kwa viongozi wa klabu, mashabiki na mtu yeyote asiyekuwa na kazi maalum kuhusiana na mchezo katika eneo la uwanja(pitch) kuwepo eneo la uwanjani ndani kuzunguka uwanja wa kuchezea(pitch)”.
Kamati inatoa Onyo na angalizo kuwa kanuni hizo zisipozingatiwa uwanja huo utafungiwa mara moja.
Tanzania Prisons ilipomenyana na Simba Uwanja wa Sokoine, ambapo zilitoshana nguvu ya bila kufungana mashabiki waliingia ndani ya Uwanja baada ya mchezo kukamilika Juni 27.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.