Home Uncategorized MTUPIAJI NAMBA MOJA KWA WAZAWA AFUNGUKA ISHU YAKE NA KOCHA MKUU PAMOJA...

MTUPIAJI NAMBA MOJA KWA WAZAWA AFUNGUKA ISHU YAKE NA KOCHA MKUU PAMOJA NA WACHEZAJI


YUSUPH Mhilu, mshambuliaji wa Kagera Sugar amesema kuwa amekuwa akipewa sapoti kubwa na Kocha Mkuu wa kikosi hicho Meck Maxime katika utendaji wa kazi yake pamoja na wachezaji wa timu hiyo.

Mhilu ni namba moja kwa utupiaji kwa wazawa ndani ya ligi akiwa ametupia jumla ya mabao 13 huku kinara akiwa ni Meddie Kagere mwenye mabao 19 anayekipiga ndani ya Simba.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mhilu amesema kuwa amekuwa akipambana kwa juhudi pale anapopata nafasi kwa kuwa amekuwa akiaminiwa na Maxime.

“Kikubwa ni uaminifu ambao upo kati yangu na kocha mbali na hilo wachezaji wote kiujumla tunaishi kwa kushirikiana jambo ambalo linatufanya tuzidi kupambana kufikia malengo yetu.

“Tunahitaji kumaliza ligi tukiwa ndani ya nafasi tano za juu na hilo linawezekana kwa kuwa tuna mechi bado zipo mkononi hizo tutapambana kupata matokeo mazuri,” amesema.

Hakuwepo kwenye kikosi kilichopoteza kwa kufungwa bao 1-0 na Yanga Uwanja wa Kaitaba kwa kuwa anasumbuliwa na majeraha ya nyama za paja.

Kagera Sugar ipo nafasi ya nane kwenye msimamo ikiwa na pointi 46 baada ya kucheza mechi 34 imebakiwa na mechi nne mkononi kukamilisha mzunguko wa pili.

SOMA NA HII  KESHO NDANI YA CHAMPIONI JUMATANO USIPANGE KUKOSA NAKALA YAKO