Home Uncategorized MUUAJI WA SIMBA APEWA JUKUMU LINGINE LA KUIMALIZA KWA MARA NYINGINE TENA...

MUUAJI WA SIMBA APEWA JUKUMU LINGINE LA KUIMALIZA KWA MARA NYINGINE TENA TAIFA


LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa kiungo wake mshambuliaji Bernard Morrison yupo tayari kuimaliza Simba kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali wa Kombe la Shirikisho unaotarajiwa kuchezwa Julai 12, Uwanja wa Taifa.
Mchezo huo umeshika hisia za mashabiki wengi unatarajiwa kuanza kutimua vumbi majira ya saa 11:00 huku mshindi wa mchezo huo atamenyana na mshindi wa robo fainali ya kwanza kati ya Sahare All Stars v Namungo itakayopigwa Uwanja wa Mkwakwani.
Morisson hakuwa kwenye kikosi kilichoivaa Biashara United Julai 5 Uwanja wa Karume kwenye sare ya bila kufungana alikwea pipa Julai 6 na kujiunga na kikosi kilichojiandaa na mchezo dhidi ya Kagera Sugar baada ya Eymael kuhitaji huduma yake.
Akizungumza na Saleh Jembe, Eymael amesema kuwa wachezaji wake wote wapo tayari kwa ajili ya mchezo dhidi ya Simba ikiwa ni pamoja na kiungo wao aliyemtungua Aishi Manula, Morrison Machi 8, Uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.
“Morrison kwa sasa yupo kwenye kikosi na yupo tayari kwa ajili ya mchezo dhidi ya Simba. Amesharejea tayari kikosini na mchezo wetu dhidi ya Kagera Sugar amefunga bao moja lililotupa ushindi mbele ya wapinzani wetu. 
“Ninajua mchezo utakuwa mgumu lakini tunahitaji kupata ushindi kwani ni muhimu kwetu kuwa hivyo.”

Leo Yanga imerejea kutoka Bukoba ambako iliweka kambi kwa muda ikiwa ni maandalizi ya mchezo wa nusu fainali dhidi ya watani zao wa jadi Simba.

Mashabiki elfu 30 tu wataruhusiwa kuingia kwenye mchezo huo kwa mujibu wa Serikali ikiwa ni hatua ya kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.
SOMA NA HII  TUSIJISAHAULISHE CORONA BADO IPO, KILICHOBAKI TUMALIZE MSIMU HUKU TUKICHUKUA TAHADHARI