Home Uncategorized MWINYI ZAHERA: MOLINGA AMEPONZWA NA BENCHI NDIO MAANA HAJAFUNGA MABAO 15

MWINYI ZAHERA: MOLINGA AMEPONZWA NA BENCHI NDIO MAANA HAJAFUNGA MABAO 15


KOCHA wa zamani wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa kama straika wa timu hiyo David Molinga asingekuwa akiwekwa benchi mara kwa mara, basi angefikisha mabao 15 kama alivyoahidi mwaka jana.

Zahera, pamoja na mambo mengine ya Yanga, alizungumzia suala la Molinga ambaye amemaliza Ligi Kuu akifunga jumla ya mabao 11, manne, pungufu ya yale aliyoahidi Zahera wakati akimsajili akitokea nchini DR Congo.
Septemba mwaka jana, akiwa kocha wa Yanga, Zahera alisema atakubali kukatwa mkono, au atatoa dola 1,000, kwa waandishi wa habari za michezo kama Molinga asipofikisha mabao 15 mpaka 20.
“Mimi nilijua kuwa atafikisha idadi hiyo ya magoli. Ni kweli hajafikisha, ilikuwa bado manne tu afikishe 15, lakini asingeweza kufikisha kama hachezeshwi.
“Kuna baadhi ya mechi wanamuacha, halafu baadaye wanamchukua, mara wanasema vibaya, mara mashabiki wanamzomea, mara wanamuambia maneno mabaya, unafikiri atafanya nini, lakini nina uhakika angecheza mechi zote na wangempa nafasi, angefikisha idadi ya hiyo na kupita pia,” alisema Zahera ambaye naye alitimuliwa kuwa kocha na klabu hiyo Novemba mwaka jana.
SOMA NA HII  VIDEO: ITAZAME NGOMA MPYA YA MBOSSO -MAAJAB

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here