Home Uncategorized WABISHI MBAO FC WAPUNGUZIWA KASI NA WAJEDA

WABISHI MBAO FC WAPUNGUZIWA KASI NA WAJEDA


JKT Tanzania leo wameipunguzia kasi Mbao FC iliyo chini ya Kocha Mkuu, Felix Miziro ya kujinasua kwenye hatari ya kushuka daraja kwa kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1.

Mchezo huo uliochezwa leo, Julai 19 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma umekamilika kwa timu hizo kugawana pointi mojamoja huku matumaini ya Mbao kubaki kwenye ligi msimu ujao yakizidi kupukutika taratibu.

Mbao FC imetoka kushinda mbele ya Simba kwa mabao 3-2 Uwanja wa Taifa jambo lililoongeza matumaini kwa Mbao kubaki ndani ya ligi kwa kua wametoka kumfunga bingwa wa ligi ila mambo leo yamekuwa tofauti.

Frank Nchimbi dakika ya 45 alianza kupeleka maumivu kwa wabishi, Mbao na kuwafanya waende mapumziko wakiwa nyuma kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili Abdulkarim Sengeja aliandika bao la kwanza kwa Mbao dakika ya 57 na kuwafanya wagawane pointi mojamoja.

Sare hiyo inawafanya Mbao wabaki nafasi ya 19 wakiwa na pointi 39 huku JKT Tanzania ikiwa nafasi ya saba na pointi 50 ina uhakika wa kubaki ndani ya ligi msimu ujao.

SOMA NA HII  YANGA YAIPA NGUVU NAMUNGO KIMATAIFA