Home Uncategorized YANGA KUTUA DAR LEO KUENDELEA KUIVUTIA KASI SIMBA

YANGA KUTUA DAR LEO KUENDELEA KUIVUTIA KASI SIMBA


KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Luc Eymael kinatarajiwa kutua leo Dar majira ya saa sita mchana kikitokea Bukoba.

Yanga ilikuwa na kazi ya kumenyana na Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambapo Yanga ilishinda kwa bao 1-0.

Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Kaitaba na bao pekee la ushindi lilifungwa na Bernard Morrison akimalizia pasi ya David Molinga.

Akizungumza na Saleh Jembe, Eymael amesema kuwa wanarejea Dar ili kuendelea na maandalizi ya mwisho ya mchezo wao dhidi ya Simba ambao ni wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho, utakaopigwa Julai 12, Uwanja wa Taifa.

“Tunarudi Dar kuendelea na maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya Simba, nina amini kwamba kila kitu kitakuwa sawa na wachezaji wapo tayari kwa ushindani,” amesema. 

Mshindi wa mchezo huo atamenyana na mshindi kati ya Sahare All Stars dhidi ya Namungo FC utakaochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

SOMA NA HII  KAZI IMEANZA CAFCL WAPINZANI WA YANGA WAMTIMUA KOCHA WAO