Home Uncategorized YANGA WATOA TAMKO KUHUSU BERNARD MORRISON

YANGA WATOA TAMKO KUHUSU BERNARD MORRISON


UONGOZI wa Klabu ya Yanga umesema kuwa suala la Bernard Morrison kiungo mshambuliaji kucheza chini ya kiwango na kuondoka baada ya dakika 64 alizotumia uwanjani linalihusu benchi la ufundi kwani wao ndio wanatambua ufiti wa kila mchezaji. 

Morrison mwenye mabao matano alitumia dakika 64 Julai 12 Uwanja wa Taifa wakati timu yake ikipoteza kwa kufungwa mabao 4-1 Kwenye mchezo wa hatua  ya nusu fainali dhidi ya Simba. 

Nafasi ya Morrison ilichukuliwa na mshambuliaji wa Yanga, Patrick Sibomana ambaya aliingia kumalizia dakika 26.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela amesema kuwa Morrison alisamehewa na mashabiki baada ya kufunga mbele ya Kagera Sugar ila kwa kushindwa kuonyesha kiwango bora kiliwakasilisha mashabiki.

“Suala la Morrison kushindwa kucheza kwa ubora hilo lipo ndani ya benchi la ufundi ambalo linatambua ni namna gani mchezaji alishindwa kuonyesha kiwango.

“Kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar alifunga bao pekee la ushindi na mashabiki walifurahi na walimsamehe ila kwa kuwa ameshindwa kuonyesha kiwango kikubwa basi anazomewa,tutalifanyia kazi,” amesema. 

Morrison baada ya kutolewa aliongoza safari mpaka nje ya uwanja ambapo alichukua bodaboda na kuelekea kusikojulikana.

SOMA NA HII  KAZE KIBARUANI LEO, KUKOSA NYOTA WAKE NANE DHIDI YA SIMBA