Home Uncategorized YANGA WATUA DAR KAMILI GADO KUELEKEA MCHEZO WAO DHIDI YA SIMBA

YANGA WATUA DAR KAMILI GADO KUELEKEA MCHEZO WAO DHIDI YA SIMBA


KIKOSI cha Yanga leo kimerejea Dar es Salaam kutoka Kagera ambapo kilikuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar. 

Yanga ilishinda kwa bao 1-0, Julai 8 lililopachikwa kimiani na Bernard Morrison kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo aliyemalizia pasi ya David Molinga. 

Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu, Luc Eymael ina kazi ya kujiandaa kumenyana na Simba kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya nusu fainali.

Eymael amesema kuwa wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa hatua ya nusu fainali dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa Julia 12, Uwanja wa Taifa.

“Tupo vizuri na tutawaandaa wachezaji kufanya vizuri kwenye mchezo wetu dhidi ya Simba ambao utakuwa na ushindani mkubwa,”.

Mshindi wa mchezo huo atakutana na mshindi wa nusu fainali ya kwanza itakayowakutanisha Sahare All Stars dhidi ya Namungo FC utakaochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kwenye fainali.

Fainali inatarajiwa kuchezwa Sumbawanga na atakayetwaa taji la Kombe la Shirikisho atapata nafasi ya kuiwakilisha nchi Kwenye mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika.

SOMA NA HII  MORRISON MWINGINE KUSHUSHWA YANGA