Home Uncategorized ZAHA ATUMIWA UJUMBE WA UBAGUZI WA RANGI

ZAHA ATUMIWA UJUMBE WA UBAGUZI WA RANGI

WILFRIED Zaha nyota anayekipiga ndani ya Klabu ya Crystal Palace amesema kuwa amepokea jumbe mbili ambazo zilikuwa zinaeleza kuhusu ubaguzi wa rangi wakati wa kuifuata Aston Villa mchezo wa Ligi Kuu England. 

Leo Julai 12, Aston Villa anakokipiga Mbwana Samatta ipo kazini kumenyana na Crystal Palace. 

Mshambuliaji huyo amesema kuwa alipokea meseji mbili ambazo zilikuwa zinambagua kutokana na rangi yake jambo lililompotezea furaha.

“Nilipokea meseji mbili ambazo zote zilikuwa zinasema kwamba sitafunga mbele ya Aston Villa kwa kuwa rangi ni nyeusi jambo ambalo sijalipenda na ni mbaya kwangu na dunia,”.

Uongozi wa Premier league umesema kuwa kwa sasa unafanyia uchunguzi suala hilo.

SOMA NA HII  KANTE NA JORGINHO WAPO KWENYE MPANGO WA KUUZWA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here