Uncategorized

RAGE:SUALA LA MORRISON JEPESI ILA MAMBO YANAKUZWA

admin August 12, 2020 11:47 am

 

MWENYEKITI wa zamani wa Simba ambaye aliwahi kuwa Makamu wa Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) Ismael Rage amesema kuwa sakata la Bernard Morrison ni jepesi ila mambo yanakuzwa kuwa makubwa.

Rage amesema:”Yanga wangeweka mkataba hadharani kama wanao. Kwangu Yanga wamepigwa bao la kisigino. Maana kuna ushahidi alicheza mechi mbili kabla ya kuwa na kibali.

“Ndio maana nimesema hili suala ni jepesi sana na ninawatahadharisha TFF, maana kuna TMS Manager ambaye anacontrol namba. Anayeingia anakuwa ana namba yako, kama ukitaka kuingia yaani yule meneja, maana yake TFF nao wanaona. 


“Sasa isije ikawa mchezo huu umechezwa na TFF wameona maana yake itakuwa fedheha kwa nchi na TFF yenyewe, ” amesema  Rage. 

Leo kesi ya Morrison inatarajiwa kutolewa hukumu baada ya kuskilizwa kwa muda wa siku tatu mfululizo.

Ilianza Agosti 10 kuskilizwa makao makuu ya TFF pale Karume ikaendelea Agosti 11 na leo Agosti 12 inaendelea kuskilizwa na majibu yanatarajiwa kutolewa leo.
MGORE KIPA NAMBA MOJA WA BIASHARA UNITED ATAJA KILICHO NYUMA YA MAFANIKIO YAKE BREAKING:FARID MUSSA ASAINI YANGA RASMI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply