Home Uncategorized BERNARD MORRISON AFUNGUKIA USAJILI WAKE SIMBA

BERNARD MORRISON AFUNGUKIA USAJILI WAKE SIMBA

BERNARD Morrisom kiungo mshambuliaji ambaye leo ametambulishwa ndani ya Simba kwa dili la miaka miwili akitokea Klabu ya Yanga amesema kuwa hakuna haja ya mashabiki kumlaumu kwa kuwa ni sehemu ya kazi yake.


Morrison alikuwa kwenye mvutano mkubwa na Yanga kwenye ishu ya mkataba ambapo yeye alikuwa anasema kuwa anamkataba wa miezi sita ambao umekwisha huku uongozi wa Yanga ukieleza kuwa bado nyota huyo alikuwa anadili la miaka miwili.


Baada ya Simba kumtangaza Morrison, Yanga nao walitoa tamko kuwa wanafuatilia suala hilo ili kujua ukweli ili wachukue hatua kuhusu suala hilo kwa kuwa bado ana mkataba mpaka 2022.


Akizungumza muda mfupi kabla ya mchezo wa hisani unaochezwa muda huu, Uwanja wa Mkapa kati ya TimuKiba na TimuSamatta huku yeye akiwa ni mchezaji wa TimuSamatta, Morrison amesema:”Najua wengi wanasema kuhusu mimi mashabiki wanakasirika lakini hakuna baya, huu ni mpira na hii ni kazi yangu.

“Naiheshimu Yanga kwa kuwa ni timu kubwa na ina uwezo mkubwa nami pia ninajua kwamba Simba ni timu kubwa na ina mashabiki wake hivyo ni mwendelezo wa kazi,” amesema. 


Chanzo:Azam TV  

SOMA NA HII  OKTOBA 26 SIMBA KAZINI TENA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here