Home Uncategorized MASHARTI WALIYOPEWA YANGA KUMPATA SURE BOY LAZIMA ‘WAVUNJE BENKI’

MASHARTI WALIYOPEWA YANGA KUMPATA SURE BOY LAZIMA ‘WAVUNJE BENKI’

 MATAJIRI wa Azam FC, wamekubali kumuachia kiungo wao mchezeshaji fundi, Salum Abubakary ‘SureBoy’ kwenda kuichezea Yanga kwa masharti ya kuweka dau kubwa mezani ili kumpata nyota huyo.

 

Yanga kwa sasa inapambana kuipata saini ya SureBoy ambapo kwa mara ya kwanza inaelezwa walipeleka dau la shilingi milioni 30 ambalo Azam waliligomea kisha wakaongeza milioni 15 na kufanya iwe milioni 45 ambazo nazo pia Azam FC ilizigomea. 

 

Yanga imedhamiria kutengeneza timu itakayokuwa na ushindani mkubwa katika msimu ujao, ikiwemo kuchukua mataji yote watakayoyashindania.

 

Mtoa taarifa amesema dau hilo la usajili la milioni 45 Azam FC wamelikataa na kuwataka waongezewe kwa kuwa SureBoy ni Icon wa timu.

 

“Yanga wamepeleka barua ya kumuhitaji Sure Boy, lakini uongozi wa Azam wanajadiliana juu ya ofa ndogo iliyopelekwa ukizingatia kwamba kiungo huyo ana uwezo mkubwa ndani ya uwanja hivyo wanachohitaji ni heshima kwa mchezaji na jina pia la Azam FC.


“Haina maana kwamba Azam hawawezi kumuachia SureBoy hapana wanaweza ila lazima Yanga wavunje benki kupata saini ya nyota huyo kwani bado ana dili la mwaka mmoja,” ilieleza taarifa hiyo.

 

Alipotafutwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam, Abdulkarim Amin ‘Popati’ kuzungumzia hilo alikiri kupokea ofa hiyo kwa kusema: “Ni kweli Yanga wamewasilisha barua pamoja na ofa yao ya kumuhitaji Sure Boy.

 

” Muda siyo mrefu tutawajibu juu ya ofa yao, lakini nichukue nafasi hii kuwapongeza Yanga kwa kufuata taratibu za usajili, walianza kwa Nchimbi (Ditram) ambaye walimuhitaji na tulimuachia kwenda huko na kwa Nchimbi pia walileta dau la kwanza lilikuwa dogo tukawarudisha baadaye tukaelewana, mpira ni biashara,” amesema.

SOMA NA HII  GAMONDI AGOMA KUSHUKA KUTOKA KILELENI ATOA KAULI HII