Home Uncategorized MTIBWA SUGAR WAFANYA MABORESHO BENCHI LA UFUNDI

MTIBWA SUGAR WAFANYA MABORESHO BENCHI LA UFUNDI


UONGOZI wa Mtibwa Sugar leo Agosti 28 umetangaza benchi lake la ufundi kwa ajili ya msimu wa 2020/2021 unaotarajiwa kuanza Septemba 6.

Zubery Rashid Katwila ataendelea kukiongozi kikosi cha Mtibwa Sugar akiwa Kocha Mkuu akisaidiana na Vicent Barnabas ambaye awali alikuwa Kocha Mkuu wa timu ya Vijana.

Barnabas alikiongoza kikosi cha timu ya vijana kutwaa ubingwa wa under 20 na kuzalisha wachezaji wengi kutoka timu za vijana hadi timu ya wakubwa na nafasi yake imechukuliwa na Awadh Juma Issa

Aidha Mtibwa Sugar imefanya mabadiliko katika nafasi ya kocha wa makipa kwa kumtambulisha Soudy Slim aliyewahi kuwa mchezaji wa Mtibwa.


Wengine ni Daktari wa timu ambaye ni Lawrance Mushi, Amir Abdallah msimamizi wa vifaa vya timu na David Chitty B’-goya ambaye ni meneja wa timu.


SOMA NA HII  KABLA YA LIGI HAIJAMALIZIKA, UBINGWA LIGI KUU WATAJWA SIMBA