Home Uncategorized NAMUNGO FC NAO WAMALIZANA NA JEMBE LA KAZI KUTOKA LIPULI ASAINI MIAKA...

NAMUNGO FC NAO WAMALIZANA NA JEMBE LA KAZI KUTOKA LIPULI ASAINI MIAKA MIWILI

FREDY Tangalo kiungo wa Lipuli, leo amesaini kandarasi ya miaka miwili ndani ya Klabu ya Namungo FC ya Lindi.

Kiungo huyo amesaini dili hilo akiwa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake kuisha ndani ya Klabu ya Lipuli yenye maskani yake Iringa na inatumia uwanja wa  Samora.

Huu ni usajili wa kwanza kwa Namungo FC ambayo inayonolewa na Kocha Mkuu, Hitimana Thiery ambaye anawania tuzo ya Kocha Bora kwa msimu wa 2019/20.

Lipuli msimu ujao wa 2020/21 itashiriki Ligi Daraja la Kwanza baada ya kushuka daraja msimu huu wa 2019/20 ikiwa nafasi ya 18 na pointi 44 baada ya kucheza mechi 38.

Namungo inaimarisha kikosi chake kwa sasa kwa ajili ya msimu ujao ambapo ina nafasi ya kushiriki mashindano ya Kimataifa itapeperusha Bendera ya Taifa ya Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho. 

Nafasi hiyo wamepata baada ya kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho na kukutana na bingwa wa ligi Simba ambaye alishinda kwa mabao 2-1 Uwanja wa Nelson Mandela, licha ya kupoteza imepata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa kwa kuwa tayari Simba itaiwakilisha nchi Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

SOMA NA HII  JULIO AAMUA KUTOA LA MOYONI JUU YA KOCHA MPYA SIMBA