Home Uncategorized NAMUNGO KUIFUATA SIMBA KWA TAHADHARI, UZI WA KESHO WATAMBULISHWA

NAMUNGO KUIFUATA SIMBA KWA TAHADHARI, UZI WA KESHO WATAMBULISHWA


HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo FC amesema kuwa ana kazi ngumu kesho mbele ya Simba ila anaamini watapambana kupata matokeo.

Kesho Namungo itashuka kwenye Uwanja wa Nelson Mandela kumenyana na Simba kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho.

Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema kuwa wanatambua kazi itakuwa ngumu kwa kuwa wanacheza na mabingwa wa Ligi Kuu Bara.

“Ukiwa unacheza na bingwa lazima uingie kwa tahadhari kubwa na akili kichwani kwani fainali siku zote ni fainali haina wepesi lazima itakuwa ngumu.

“Ninawaheshimu wapinzani wangu kwa kuwa nimewahi kukutana nao licha ya kwamba wachezaji wangu wengi ni wagonjwa tutafanya vizuri,” amesema.

Namungo ilifanikiwa kutinga hatua ya fainali baada ya kushinda hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa bao 1-0 mbele ya Sahare All Stars mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Mtupiaji wa bao la ushindi kwenye mchezo wa nusu fainali Edward Manyama kuna hatihati akakosa mchezo wa kesho kwa kuwa ni miongoni mwa wachezaji wanaoumwa.

Pia leo walitambulisha jezi watakazotumia kesho kwenye mchezo wa fainali unaotarajiwa kupigwa majira ya saa 9:00 alasiri.

SOMA NA HII  DAU LA KIUNGO ANAYEWINDWA NA YANGA ACHA KABISA, AKUBALI KUTUA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here