Home Uncategorized POGBA AKUTWA NA VIRUSI VYA CORONA

POGBA AKUTWA NA VIRUSI VYA CORONA

PAUL Pogba, kiungo wa Klabu ya Manchester United imeripotiwa kuwa amekutwa na Virusi vya Corona muda mfupi kabla ya msimu mpya wa Ligi Kuu England kuanza.

Kiungo huyo wa kati, raia wa Ufaransa ameondolewa kwenye kikosi cha timu yake ya Manchester United baada ya kukutwa na Virusi vya Corona.

Pia nyota mwingine wa Tottenham, Tanguy Ndombele naye pia amekutwa na Corona muda mfupi kabla ya kuingia kambini.

Pogba mwenye miaka 27 alitumia muda mwingi wa mapumziko ya ligi akiwa na familia yake hivyo atakuwa kwenye uangalizi kwa muda mpaka pale atakaporejea kwenye ubora wake kwa muda wa siku 10.

Ole Gunnar Solskjaer, Kocha Mkuu wa United anatambua kuwa atamkosa nyota huyo ndani ya Old Trafford kwa kuwa ni utaratibu muhimu wa kufuatwa ili kuwakinga wachezaji wengine wasipate Virusi vya Corona.


 

SOMA NA HII  KOCHA WA YANGA AZUIWA KURUDI TANZANIA NA MFALME WA UBELGIJI