Home Uncategorized SALIBOKO AJIFUNGA MWAKA MMOJA POLISI TANZANIA

SALIBOKO AJIFUNGA MWAKA MMOJA POLISI TANZANIA


DARUESH Saliboko nyota wa Lipuli FC ya Iringa inaelezwa kuwa amemalizana na timu ya Polisi Tanzania kwa kusaini dili la mwaka mmoja licha ya mwenyewe kufanya siri.

Nyota huyo ambaye amekuwa na urafiki mkubwa na nyavu akitupia mabao 11 alikuwa na ofa tatu mkononi jambo lililomfanya aibukie ndani ya Polisi Tanzania.

Habari zinaeleza kuwa kwa sasa Saliboko ni mali ya Polisi Tanzania inayonolewa na Malale Hamsini hivyo ana uhakika wa kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara kwa kuwa Lipuli itashiriki Ligi Daraja la Kwanza.

Akizungumza na Saleh Jembe, Saliboko amesema kuwa amekuwa akiskia kuhusu suala lake la kuibukia Polisi Tanzania ila bado halijakamilika.

“Nami ninaskia kwamba ninahitajika na Polisi Tanzania ila inakuja hivi kama inakataa,” aliongea nyota huyo akigoma kuweka wazi juu ya dili lake jipya.

SOMA NA HII  NINJA ALIPWA MSHAHARA WA BILIONI 2 MAREKANI, ATACHEZA NA ZLATAN LA GALAXY