Home Uncategorized SIMBA LEO KUKIPIGA DHIDI YA KMC NA TRANSIT CAMP, MUGALO KUZIKOSA ZOTE...

SIMBA LEO KUKIPIGA DHIDI YA KMC NA TRANSIT CAMP, MUGALO KUZIKOSA ZOTE MBILI

 


KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck akishirikiana na Selaman Matola, leo Agosti 26  kitacheza mechi mbili za kirafiki.

Itacheza dhidi ya KMC na Transit Camp Uwanja wa Uhuru na itakosa huduma ya mshambuliaji wao mpya, Chris Mugalu raia wa Congo ingizo jipya kutoka Lusaka Dynamos ambaye jana alisepa kuelekea nchini Congo.

Mechi hizi mbili ni kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa Agosti 30, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha dhidi ya Namungo pamoja na mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ligi inatarajiwa kuanza Septemba 6 ambapo Simba mchezo wake wa kwanza itakuwa dhidi ya Ihefu, pale Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

 

SOMA NA HII  MABINGWA SIMBA WALIVYOINGIA KWA WADHAMINI WAO SPORTPESA NA KUKABIDHI KOMBE, WAO WAKAONDOKA NA MKWANJA