Home Uncategorized SIMBA YAAGIZA GPS ZA WACHEZAJI, LENGO KUWAFUATILIA KILA HATUA

SIMBA YAAGIZA GPS ZA WACHEZAJI, LENGO KUWAFUATILIA KILA HATUA


MWENYEKITI wa Bodi ya Klabu ya Simba na Mwekezaji Mohammed Dewji amesema ameagiza vifaa kwa ajili ya kuwamonitor wachezaji wake (GPS). 

Mo amesema hayo leo, Agosti 21 kwenye mkutano na Waandishi wa Habari akisema kuwa malengo ya kufanya hivyo ni kujua mienendo ya wachezaji ndani na nje ya uwanja.

Ameongeza kuwa malengo ya Simba kwa msimu huu ni kuweza kufika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Malengo yetu sasa ni kuendelea kushindana ndani na kushinda ubingwa lakini pia kufika kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Mipango yetu mwaka huu ni kujenga hosteli za timu, uwekezaji wa GPS ambao tutakuwa tunaona takwimu za wachezaji.


” Vifaa hivyo vitaweza kutoa taarifa kuhusu mwenendo wa mchezaji, amelala saa ngapi, mapigo yake ya moyo, kama akitumia kilevi na sehemu aliyopo pamoja na vitu vingine vingi,” amesema.

SOMA NA HII  UJUMBE WA JEMBE KUHUSU SHIGONGO