Home Uncategorized SIMBA YAKUBALI MAJEMBE YA KAZI YA YANGA

SIMBA YAKUBALI MAJEMBE YA KAZI YA YANGA

 


MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’, amesema wapinzani wao Yanga na Azam nao wamefanya usajili mzuri, hivyo kutakuwa na ushindani mkubwa msimu ujao lakini akasisitiza watapambana nao na wasahau kuchukua ubingwa kwani wamepanga kuutetea.

 

Mo ameongeza kuwa nje ya kushindana na kutwaa ubingwa wa ligi lakini pia jicho lao ni kupambana katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Wapinzani wa Simba, Yanga wao hadi sasa wameshasajili zaidi ya wachezaji nane ikiwa ni pamoja na, Mghana Michael Sarpong, Mcongo Tuisila Kisinda, Farid Mussa, Mcongo Mukoko Tonombe na Bakari Mwamnyeto.

 

Kwa upande wa Azam FC, wao wamezipata saini za Awesu Awesu, Mnyarwanda Ally Niyonzima, Mzimbabwe Prince Dube, Ismail Azizi na Danny Lyanga.

 

Mo amesema kuwa licha ya usajili huo wa wapinzani wao walioufanya kuwa mzuri, lakini wasifikirie juu ya ubingwa kutokana na kwamba wao wanalitaka kombe hilo.

 

“Tunataka kushindana kwenye ligi na tunajua wenzetu wamesajili vizuri na tuko tayari kushindana nao.

 

“Lakini malengo yetu ni kushinda ligi kwa mara nyingine tena na kupambana kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, tunataka kufika mbali safari hii, tofauti na ilivyokuwa kwa msimu uliopita,” alimaliza Mo.

SOMA NA HII  UTATA WA BAO LA MEDDIE KAGERE DHIDI YA NAMUNGO, MATAMKO YATOKA - VIDEO