Home Uncategorized SIMBA YAWEKA REKODI NDANI YA MSIMU WA 2019/20, YAKUSANYA MATAJI MATATU

SIMBA YAWEKA REKODI NDANI YA MSIMU WA 2019/20, YAKUSANYA MATAJI MATATU


KLABU ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck leo imetwaa taji lake la tatu ndani ya msimu wa 2019/20.

Simba ilianza na ngao ya jamii, kwa ushindi wa mabao 4-2 mbele ya Azam FC Uwanja wa Taifa ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Patrick Aussems.

Ilianza mechi zake 10 za  Ligi Kuu Bara chini ya Aussem kisha ikamlaiza na Sven ambaye alitwaa taji la Ligi Kuu Bara.

Simba ilitwaa taji hilo ikiwa na pointi 79 huku ikiwa na mechi sita mkononi ambazo imezikamilisha na kufanya iwe namba moja na pointi 88 kibindoni.

 Leo Agosti 2 imetwaa taji la Kombe la Shirikisho kwa ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Namungo FC.

Fainali ya leo iliyoshuhudiwa na mashabiki wengi ndani ya uwanja huo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Habari, Juliana Shonza ambaye alikuwa kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.  

Sven amesema:”Ninafuraha ndani ya moyo kwa kuwa timu imeshinda na tumefikia malengo ambayo tulikuwa tumejiwekea, haikuwa kazi rahisi kufika hapa.”

SOMA NA HII  YANGA WATAJA SABABU YA KUZITAKA POINTI TATU ZA MTIBWA SUGAR LEO