Home Uncategorized YANGA WATAJWA KUINGIA ANGA ZA AUSSEMS

YANGA WATAJWA KUINGIA ANGA ZA AUSSEMS

 Inaelezwa kuwa Patrick Aussems ambaye aliwahi kuinoa Simba yupo kwenye  hesabu za kutua ndani ya Yanga ambao kwa sasa wanamtafuta Kocha Mkuu ambaye atabeba mikoba ya Luc Eymael. 

Eymael alifutwa kazi ndani ya Yanga, Julai 27 baada ya kutoa taarifa zilizokuwa na viashiria vya ubaguzi wa rangi kwa mashabiki pamoja na viongozi. 

Mechi yake ya mwisho ilikuwa Julai 26 ambapo aliwatungua Lipuli FC, Uwanja wa Samora na ushindi huo uliipa nafasi timu hiyo kumaliza Ligi Kuu Bara ikiwa nafasi ya pili.

Habari zinaeleza kuwa miongoni mwa wanaotajwa kuwa kwenye hesabu za kuibukia Yanga ni pamoja na Aussems. 

“Kwa sasa mchakato unaoendelea ni kumsaka mbadala wa Eymael kwani timu inaingia kambini mapema kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao hivyo ni lazima aje kocha mwenye uzoefu na ligi wapo wengi ambao wanahitaji kazi jina lake litawekwa wazi karibuni,  kuhusu Aussems hilo litajulikana,”.

Yanga inaanza mazoezi leo Agosti 10 kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2020/21

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrik Mwakalebela amesema kuwa bado mchakato wa kutafuta kocha unaendelea.

SOMA NA HII  KIPA MWADUI: GOLI LA PILI SIMBA LILIKUWA OFFSIDE - VIDEO