Home Uncategorized BAYERN MUNICH WAPIGWA 4G LEO

BAYERN MUNICH WAPIGWA 4G LEO


 KLABU ya Bayern Munich leo Septemba 27 imenyooshwa kwa kuchapwa mabao 4-1 mbele ya Hoffenheim mchezo wa Bundesliga uliochezwa Uwanja wa Rhein-Neckar.

Mabao ya Hoffenheim yalipachikwa na Ermin Bicakcic dakika 16, Mu’nas Dabbur dakika ya 24 na Andrej Kramaric alipachika mabao mawili dakika ya 77 na 90+2 kwa mkwaju wa penalti.

Bao la Bayern Munich lilipachikwa kimiani na Joshua Kimmich dakika ya 36, Munich walikikwaa kisiki cha mpingo leo kwa kushindwa kuonyesha makeke yao.

Mara ya mwisho Bayern Munich kupoteza mchezo ndani ya dakika 90 ilikuwa ni Januari 11 mwaka huu na ilichapwa mabao 5-2 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Numberg.

Hivi karibuni iliwashushia kichapo cha maana Barcelona cha mabao 8-2 kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya jambo lililopelekea Lionel Messi kutishia kusepa ndani ya La Liga ila kwa sasa bado yupo ndani ya Barcelona.

SOMA NA HII  MBELGIJI WA YANGA KWENYE MTIHANI MWINGINE MGUMU LEO