Home Uncategorized KICHAPO CHA MABAO 5-2 WALICHOPOKEA CITY GUARDIOLA ASEMA NI PRESHA

KICHAPO CHA MABAO 5-2 WALICHOPOKEA CITY GUARDIOLA ASEMA NI PRESHA


 PEP Guardiola, Kocha Mkuu wa Manchester City amesema kuwa hawakutengeneza nafasi nyingi kwenye mchezo wao dhidi ya Leicester City uliochezwa jana,Septemba 26 wakati ikifungwa mabao 5-2.

Guardiola amesema kuwa walianza mchezo huo wakiwa na presha kubwa ya kutafuta matokeo jambo ambalo liliwapa wakati mgumu wachezaji wake kusaka ushindi kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Etihad.

Manchester City walianza kufunga bao dakika ya nne kupitia kwa Riyad Mahrez na lile la pili lilifungwa na Nathan Ake dakika ya 84 na yale ya Leicester City yalifungwa na Jamie Vardy aliyepiga hat trick dk ya 37(p), 53 na 58b(p), James Maddison dk 77 na Youri Tielemans dk 88,(p).

Kocha huyo amesema kuwa wana kazi kubwa ya kufanya ndani ya Ligi Kuu England ili kuwa bora na imara kwenye mechi zijazo.

“Tulikiwa na presha kubwa kwenye mchezo wetu na wachezaji walijitahidi kutafuta ushindi ila mambo ndo yakawa hivyo,”.

SOMA NA HII  SIMBA YATUA KWA STARAIKA HUYU MKONGO