Home Uncategorized M-Bet TANZANIA YATOA MAMILIONI KWA WATANZANIA WAWILI

M-Bet TANZANIA YATOA MAMILIONI KWA WATANZANIA WAWILI


 MASHABIKI wa soka wawili nchini kila mmoja ameshinda kiasi cha Sh 79, 465, 240 baada ya kubashiri  kwa usahihi matokeo ya mechi 12 za ligi mbalimbali duniani.

Mashabiki hao ni Felix George Simba na Twalib Mfingile ambao wameshinda kupitia mchezo wa Perfect 12 unaoendeshwa na kampuni ya michezo ya kubahatisha ya M-Bet Tanzania.

Meneja masoko wa M-Bet Tanzania, Allen Mushi amesema kuwa washindi hao wawili wameshinda jumla ya sh 159,930,480.

Mushi amesema kuwa kampuni yao itaendelea kuwa nyumba ya mabingwa kwani washindi hao wawili ni wa tano tokea kuanza kwa msimu huu.

“Kama tulivyosema kuwa kushinda na M-Bet ni simple tuu na Mfingile na Simba wamedhihirisha kuwa kushinda na suala rahisi sana kutokana na aina ya mechi ambazo M-BET imekuwa ikizichagua kwa ajili ya mashabiki wa soka kubashiri,” amesema Mushi.

Amesema kuwa M-BET inajivunia kuwawezesha Watanzania kwa kubadilisha maisha yao ambapo mpaka sasa jumla ya washindi watano wamepatikana kupitia michezo yao ya kubashiri,” amesema Mushi.

Kwa upande wake, Mfingile amesema kuwa atatumia fedha hizo kwa kilimo cha kisasa na masuala mengine ya maendeleo katika familia yake.

“Mimi ni shabiki wa mpira lakini si kwa timu za Tanzania, napendelea zaidi timu za Ulaya na ndiyo nimeshinda kwa kutokana na kuzifuatilia kwa ukaribu sana,” amesema Mfingile ambaye ni mkazi wa Ifaraka, mkoani Morogoro.

Kwa upande wake, Simba amesema kuwa amejisikia faraja sana kubashiri na kushinda hasa kwa timu yake ya Arsenal ambayo inatamba sana kwenye Ligi Kuu ya England.

“Huwa Napata ugumu sana kutabiri mechi za Manchester United, hata hivyo nilifanikiwa kubashiri matokeo yake, Arsenal ni kushinda tu,” amesema Simba ambaye ni daktari mkoani Ruvuma.

Ofisa Mamlaka Mapato  (TRA) mkoa wa Ilala, Shaaban Mwanga amesema kuwa mashabiki hao watakatwa asilimia 20 kama kodi ya Serikali.

Mwanga aliipongeza M-Bet kwa kuwa walipa kodi wa zuri nchini.

SOMA NA HII  SIMBA: TUNAPITIA KIPINDI KIGUMU KWA SASA