Home Uncategorized MUANGOLA WA YANGA KUMCHOMOA KIUNGO NDANI YA KIKOSI CHA KWANZA

MUANGOLA WA YANGA KUMCHOMOA KIUNGO NDANI YA KIKOSI CHA KWANZA


 UPO uwezekano mkubwa kiungo mmoja kati ya watano waliokuwepo kwenye kikosi cha kwanza cha Mserbia, Zlatko Krmpotic nafasi yake kuchukuliwa na kiungo Carlos Carlinhos.

 

Hiyo ni siku chache baada ya Carlinhos, raia wa Angola kucheza kwa kiwango na kuisaidia timu yake ya Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Septemba 13, Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Kiungo huyo katika mchezo huo aliingia uwanjani dakika ya 60, akatoa asisti iliyozaa bao pekee lililofungwa na Lamine Moro kwa kichwa na Yanga kushinda 1-0.Staa huyo mpya ndani ya kikosi cha Yanga, aliingia uwanjani akichukua nafasi ya kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ na kufanya balaa hilo.


Muangola huyo anatajwa kuingia katika kikosi cha kwanza akichukua nafasi moja kati ya viungo waliokuwepo katika kikosi cha kwanza ambao ni Haruna Niyonzima, Tuisila Kisinda, Fei Toto na Deus Kaseke anayetajwa kuwa chaguo la kwanza kutoka kikosini.

 

Akitokea benchi, kiungo huyo alifanikiwa kupiga mashuti manne, kona tano, kati ya hizo moja ilizaa bao baada ya kuichonga kiufundi kabla ya kuingia wavuni na kuiwezesha timu yake kupata pointi tatu.


Akizungumzia nafasi ya kiungo huyo, Krmpotic amesema: “Carlinhos ni mchezaji mzuri mwenye uwezo mkubwa ambaye ana faida nyingi katika timu, lakini nimekuwa nikimuanzisha nje kutokana kutofanya mazoezi kwa zaidi ya miezi minne.

 

“Hiyo ni baada ya ligi ya nchini kwao Angola kufutwa, hivyo ninahofia kumuharibia uwezo wake, alikuwa na program maalum kwa ajili ya kumuongezea fitinesi ambayo tayari imemalizika.


“Hivyo, ninatarajia kuanza kumtumia katika kikosi cha kwanza kwenye michezo inayofuata kwani kadiri siku zinavyokwenda ndiyo anazidi kubadilika.”

SOMA NA HII  HIZI NDIZO REKODI MATATA ZA SIMBA NA UBINGWA WAKE MSIMU 2019/20