Home Uncategorized MUGALU ACHEKELEA MAISHA NDANI YA SIMBA

MUGALU ACHEKELEA MAISHA NDANI YA SIMBA


MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu amesema kuwa anafurahi maisha anayoishi ndani ya Simba kwa sasa baada ya kuibukia ndani ya kikosi hicho akitokea Klabu ya Lusaka Dynamo ya Zambia.


Akiwa ndani ya Simba kwa msimu wa 2020/21 amecheza mechi tatu za ushindani na kufunga mabao matatu ambapo amefunga mawili kwenye mechi za kirafiki ilikuwa ule wa Vital’O na ule dhidi ya African Lyon na kwenye ligi alifunga mbele ya Biashara United.

Mugalu amesema:” Nafurahia maisha ndani ya Simba, tangu siku ya kwanza nimefika walinipokea vizuri na hadi sasa tunaishi vizuri. Namshukuru Mungu kwa hilo.” amesema.

Kesho, Septemba 26 Simba ina kibarua cha kumenyana na Gwambina FC mchezo wa ligi utakaopigwa Uwanja wa Mkapa.


Simba imetoka kushinda mabao 4-0 mbele ya Biashara United inakutana na Gwambina FC ambayo imetoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Ruvu Shooting jambo linaloongeza ugumu wa mchezo.


Kwenye msimamo, Simba ipo nafasi ya tatu na pointi saba  huku Gwambina FC ikiwa nafasi ya 14 na pointi moja baada ya kupata sare ya bila kufungana na Kagera Sugar.

SOMA NA HII  SIMBA YAFUNGUKIA ISHU YA UNAHODHA