Home Uncategorized OLE GUNNAR AMWAMBIA SANCHO KABLA DIRISHA LA USAJILI HALIJAFUNGWA ATAIBUKIA UNITED

OLE GUNNAR AMWAMBIA SANCHO KABLA DIRISHA LA USAJILI HALIJAFUNGWA ATAIBUKIA UNITED


MANCHESTER United inasemekana wana imani watamsajili Jadon Sancho kabla ya dirisha la usajili kufungwa.


Meneja wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amemwambia nyota wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho kuwa dili lake la kujiunga na United litakamilika kwa mujibu wa ripoti ya Dagbladet.

Mpaka sasa United walishindwa kutoa fedha ya pauni milioni 108 ambayo Dortumund wanahitaji ili wamuachie kiungo Sancho mwenye uwezo mkubwa ndani ya uwanja.

Dirisha la usajili  litafungwa Oktoba 5 lakini, Solskjaer anaonekana kuwa na ujasiri wa wa kumpata Sancho ambae ndio tageti yake ya kwanza msimu huu.

Miongoni mwa dili ambalo limezungumzwa kwa muda wote na halijaonesha mafanikio ndani ya united ni la nyota huyu aliyefunga jumla ya mabao 20 msimu uliopita na kutoa pasi 20 kwenye mashindano yote. 

SOMA NA HII  GWAMBINA YAPOTEZA POINTI TATU MBELE YA BIASHARA UNITED

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here