Home Uncategorized ARSENAL YAPINDUA MEZA

ARSENAL YAPINDUA MEZA

 


ARSENAL imeanza kwa ushindi wa mabao 2-1 ndani ya kundi B kwenye Kwenye mashindano ya Europa League baada ya kupindua meza kibabe wakitokea nyuma na kushinda mabao 2-1 dhidi ya Rapid Wien.


Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Allianz Stadion Taxiarchis Fountas alianza kupachika bao la Kwanza kwa Rapid Wien lililopinduliwa na David Luis dakika ya 70.


Bao la pili na la ushindi lilipachikwa na nahodha Pierre Emerick Aubameyang dakika ya 74 na kuifanya Arsenal kusepa na pointi tatu jumlajumla wakiwa ugenini.


Mikel Arteta Kocha Mkuu wa Arsenal amesema kuwa anafurahi kuona vijana wake wanashinda na kuwataka waongeze juhudi zaidi katika kuboresha viwango vyao.

SOMA NA HII  LIVERPOOL WACHEKELEA KUTWAA UBINGWA WAO BAADA YA MIAKA 30

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here