Home Uncategorized KAZE NA WINGA MPYA WATAJWA KUWA SABABU YA YANGA KUTWAA UBINGWA

KAZE NA WINGA MPYA WATAJWA KUWA SABABU YA YANGA KUTWAA UBINGWA


 MKUU wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano kutoka Shirikisho la Soka la Burundi (FFB), Ramadhan Kabugi, amefunguka kuwa kitendo cha Yanga kumsajili Said Ntibazonkiza pamoja na kumpa ajira mwalimu Cedric Kaze, kitaisaidia timu hiyo kutwaa kombe la ligi msimu huu na kuweka rekodi ya kipekee kwenye Ligi Kuu Bara.

 

Kabugi alisema Ntibazonkiza ni mchezaji mkongwe na mzoefu kwenye soka la ushindani kwa kuwa ameshacheza kwenye ligi kubwa za Ulaya, lakini mbali na hivyo ni mtu mpambanaji anayekuja kutibu tatizo la uhaba wa mabao ndani ya Yanga.

 

Huku akiongeza kuwa Kaze ni kocha ambaye ubora wake ni wa juu na utaipa mafanikio Yanga, kitu kizuri zaidi anakwenda kuungana na Ntibazonkiza ambaye alishawahi kufanya naye kazi miaka ya nyuma.


Akizungumza na Championi Ijumaa, Kabugi amesema: “Yanga wamefanya usajili mzuri sana, kwa sababu Ntibazonkiza ni mchezaji mwenye kiwango, lakini mbali na hivyo ni mpambanaji akiwa uwanjani.

 

“Unaweza ukaona alivyocheza dhidi ya Tanzania, pale alikuwa amekaa miezi minne bila kucheza mechi ya ushindani.

 

“Sasa akikaa na Yanga akafanya mazoezi na kuelewana na wenzake vizuri, bila shaka anakwenda kuwapa ubingwa Yanga ambao wameukosa kwa miaka mitatu sasa,” alisema Kabugi na kuongeza:“Kuhusu ujio wa Kaze ni faida nyingine kwa Yanga kwani ni kocha mzuri na akiungana na Ntibazonkiza, timu hiyo itafanikiwa sana,” alisema Kabugi.

SOMA NA HII  NCHIMBI: PROGRAMU YA KOCHA MKUU ITANIRUDISHA KWENYE UBORA WANGU