Home Uncategorized KMC YAANZA KUIVUTIA KASI YANGA MWANZA

KMC YAANZA KUIVUTIA KASI YANGA MWANZA


 KIKOSI cha KMC kimeshaweka kambi Mwanza kwa sasa kwa ajili ya kujiwinda na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga utakaochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.


KMC itashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Ruvu Shooting uliochezwa Uwanja wa Uhuru.


Kikosi kilikwea pipa jana na kuibukia Mwanza kwa ajili ya mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 25, saa 10:00 jioni.


Inakutana na Yanga ya Cedric Kaze ambayo imetoka kushinda bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania, Uwanja wa Uhuru.


Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na wanaamini wataibuka na ushindi kwenye mchezo huo mgumu.


“Kikosi kipo sawa na kinaendelea na mazoezi ili kujiweka sawa kwa ajili ya mechi yetu dhidi ya Yanga, kila mchezaji anatambua majukumu yake na utayari ni mkubwa.


“Kushindwa kwetu kupata matokeo mbele ya Ruvu Shooting haina maana kwamba tumeshindwa hapana hatujakata tamaa na tutaendelea kupambana kwa ajili ya mechi zetu zijazo,” amesema.

SOMA NA HII  BREAKING: BEKI MWILI JUMBA AMLIZANA NA SIMBA LEO MIAKA MIWILI