Home Uncategorized NAMUNGO FC: TATIZO LIPO KWENYE MAANDALIZI

NAMUNGO FC: TATIZO LIPO KWENYE MAANDALIZI


 HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Klabu ya Namungo FC amesema kuwa tatizo linaloisumbua timu hiyo kwa sasa ni kushindwa kupata maandalizi mazuri mwanzoni mwa msimu.

Msimu wa 2020/21 timu nyingi zilipata muda mchache wa maandalizi kutokana na uwepo wa janga la Corona ambalo lilivuruga ratiba nyingi duniani.

Namungo ikiwa imecheza jumla ya mechi 7, imeshinda mechi tatu, imepoteza mechi nne ikiwa nafasi ya nane kwenye msimamo na pointi zake ni tisa.

“Tumekuwa na matatizo kidogo kwenye mwanzo wa msimu hasa baada ya kuona kwamba tulishindwa kuwa na maandalizi mazuri mwanzo mwa msimu.

“Ila mpaka sasa hapa tulipo sio sehemu mbaya kwani tmu inapambana na inapata matokeo pale inapohitajika tutafanya vizuri mashabiki watupe sapoti.

“Kupoteza kwa mpira wa adhabu huwezi kulaumu wachezaji kwani hilo ni jambo ambalo hakuna anayetarajia labda kwa kuwa wameshindwa kupata matokeo ni jambo la kutazama pale ambapo tumekosea ili tuweze kufanya vizuri mechi zijazo,” amesema.

Jana Oktoba 19, Namungo FC ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Kwa matokeo hayo yanaifanya Mtibwa Sugar, ifikishe jumla ya pointi nane ikiwa nafasi ya 12 baada ya kucheza mechi saba za ligi.

SOMA NA HII  KOCHA ARSENAL HANA HOFU YA KUCHIMBISHWA