Home Uncategorized SADIO MANE AKUTWA NA CORONA

SADIO MANE AKUTWA NA CORONA


MSHAMBULIAJI matata ndani ya kikosi cha Liverpool, Sadio Mane raia wa Senegal ambaye anafanya vizuri kimataifa amekutwa na Virusi vya Corona baada ya kufanyiwa vipimo.


Uongozi wa Liverpool umeweka wazi kwamba nyota huyo kwa sasa anatibu Virusi vya Corona na ametengwa na wenzake ili kupunguza maambuzi zaidi na alibainika bila kuonyesha dalili zozote zile.

Mane anakuwa mchezaji wa pili chini ya Kocha Mkuu, Jurgen Klopp kukutwa na Virusi vya Corona baada ya nyota wao mpya, Thiago Alcantara  kukutwa naye ana Corona mapema mwanzoni mwa wiki hii.

Taarifa rasmi kutoka ndani ya Klabu ya Liverpool ambao ni mabingwa watetezi wa taji la Ligi Kuu England imesema kuwa kwa sasa wachezaji wake wote wanafuata taratibu zilizowekwa ili kurejea kwenye ubora wao na waendelee kwenye majukumu ya kupambania taji lao.

“Sadio Mane  amekutwa na Virusi vya Corona baada ya kufanyiwa vipimo hivyo ametengwa na wengine kwa mujibu wa taratibu zilizopo na kila kitu kuhusu  yeye  na afya yake kinatazamwa kwa ukaribu.

“Nyota huyo alianza kwenye ushindi wa mabao 3-1 mbele ya Arsenal hakuonyesha dalili zozote za Corona anajihisi vizuri muda wote hata Thiago pia yupo vizuri tutaendelea kutoa taarifa zao,” ilieleza taarifa hiyo.

Mane amesema kuwa:”Habari mashabiki zangu, nimepimwa na kukutwa na Virusi vya Corona lakini kwa sasa ninaendelea vizuri na nitarudi imara zaidi ya nilivyokuwa mwanzo, msiogope.”


SOMA NA HII  JUMA ABDUL APATWA NA PIGO KUBWA, AFIWA NA MAMA YAKE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here