Home Uncategorized TAIFA STARS YAIVUTIA KASI BURUNDI

TAIFA STARS YAIVUTIA KASI BURUNDI

 


KIKOSI cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kinaendelea na maandalizi ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa ulio kwenye kalenda ya Fifa.


Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Oktoba 11, Uwanja wa Mkapa ikiwa leo ni Oktoba 7 zimebaki siku tatu kabla ya mchezo kupigwa.

Kocha wa Taifa Stars, Ettiene Ndayiragije amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na wanaamini watapata matokeo mbele ya wapinzani wao.

Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta amesema kuwa wachezaji waliochaguliwa wapo vizuri na watapambana kupata ushindi.

“Furaha kubwa ya mashabiki ni kupata ushindi hata sisi pia wachezaji tunahitaji ushindi hivyo mashabiki watupe sapoti tutafanya vizuri,” amesema.
SOMA NA HII  MO: SITISHIKI NA WANAONIPIGA VITA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here