Home Uncategorized CECAFA U 20 KUFANYIKA NOVEMBA 22 ARUSHA

CECAFA U 20 KUFANYIKA NOVEMBA 22 ARUSHA


BARAZA la Michezo Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limetangaza michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 itataanza kutimua vumbi Novemba 22 jijini Arusha.


Rais wa CECAFA ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Wallace Karia amesema michuano itashirikisha nchi tisa huku nchi mbili zikishindwa kushiriki.


Karia amesema michuano hiyo ilikuwa ifanyike Aprili mwaka huu nchini Sudan lakini kutokana na kuibuka na homa ya mafua ya Corona (COVID 19) ikabidi kuahirishwa na ndio yatafanyika mwishoni mwa wiki hii.


Karia ameongeza michuano hiyo itakuwa na vituo viwili vya Arusha na Karatu huku timu zikigawanywa kwenye makundi matatu.


Timu zitakazo shiriki ni wenyeji Tanzania, Zanzibar, Somalia, Djibouti, Kenya, Uganda, Burundi, Ethiopia na Sudan Kusini huku Eritrea na Rwanda ndio pekee ambao hawata shiriki.

SOMA NA HII  SIMBA NA YAHYA MBEGU MPAKA KIELEWEKE