Home Uncategorized DAKIKA 180, DABI YA YANGA NA SIMBA YATAWALIWA NA PENALTI TATA

DAKIKA 180, DABI YA YANGA NA SIMBA YATAWALIWA NA PENALTI TATA

 


DABI ya Kariakoo kwa misimu miwili imegubikwa na maamuzi tata kuhusu penalti kwenye mechi zote mbili za mzunguko wa kwanza.

Novemba 7, Uwanja wa Mkapa licha ya kuwepo jumla ya waamuzi sita ambapo mmoja alikuwa ni wa kati ambaye ni Abdalah Mwinyimkuu pamoja na waamuzi wengine wawili waliokuwa pembeni ya magoli pamoja na wale wawili washika vibendera bado walianguka kwenye mtengo wa msimu uliopita.

Kwenye mchezo huo ambao ulishuhudia dakika 90 ngoma ikikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1, bao la kwanza la Yanga lilifungwa na Michael Sarpong kwa  mkwaju wa penalti baada ya Joash Onyango beki wa Simba kuonekana akimchezea faulo Tuisila Kisinda nje kidogo ya 18 na likafunikwa tuta.

Ikumbukwe pia, Januari 4,2019 Uwanja wa Mkapa licha ya uwepo wa waamuzi sita na mwamuzi wa kati kuwa ni Jonesia Rukya alitoa penalti kwa Simba iliyofungwa na Meddie Kagere ambaye alionekana kuchezewa faulo na Kelvin Yondani nje kidogo ya 18.

Kwenye dabi hiyo ya mzunguko wa kwanza ngoma ilikamilika 2-2 na baada ya mchezo huo waamuzi hao ikiwa ni pamoja na Jonesia walipewa onyo na Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) kwa kushindwa kutafsiri sheria 17 za mpira.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi Tanzania, Soud Abdi Mohamed amesema kuwa jopo la wataalamu wa masuala ya waamuzi litakaa kujadili na kupitia masuala yote ambayo yametokea kwenye mechi za ligi ikiwa ni pamoja na mchezo wa dabi.

SOMA NA HII  JONAS MKUDE ATAJA CHIMBO LAKE LILIPO