Home Uncategorized HAALAD AWAFUNIKA SANCHO, ANSU, FODEN

HAALAD AWAFUNIKA SANCHO, ANSU, FODEN

ERLING Haaland amemshinda mchezaji mwenzake ndani ya Klabu ya Borusia Dortmund, Jadon Sancho kwenye tuzo ya Golden Boy baada ya kufanikiwa kuinyakua nyota.

Tuzo hiyo ya Golden Boy ilianzishwa na gazeti la nchini Italia linaloitwa Tuttosport na imekuwa ikitolewa kwa wachezaji vijana chini ya miaka 21 ambao wamekuwa wakipambania tuzo hiyo.


Haaland alifunga jumla ya mabao  44 kwenye mashindano yake yote aliyoshiriki kwa msimu wa 2019/20 alipokuwa ndani ya Klabu ya RB Salzburg ambapo alicheza jumla ya mechi 28 kabla ya  kuibukia ndani ya Klabu ya Dortmund.


Nyota mwingine ambaye alikuwa anashindana naye ni  kutoka ndani ya Klabu ya Atletico Madrid, Joao Felix  ambaye alikuwa mshindi wa tuzo hiyo msimu wa 2019.

Haalad amemshinda mchezaji mwenzake wa  Dortmund, Sancho, ambaye ni mshambuliaji pamoja na nyota kutoka Barcelona Ansu Fati  na mshambuliaji wa Manchester United  Mason Greenwood.

Pia nyota wa Bayern Munich, Alphonso Davies na yule wa Manchester City Phil Foden walikuwa kwenye mchakato wa kuwania tuzo hiyo.

Matthijs de Ligt  alitwaa tuzo hiyo 2018 na Kylian Mbappe alitwaa msimu wa  2017.

Wayne Rooney, Paul Pogba na Lionel Messi nao pia waliwahi kushinda tuzo hiyo.

Haaland alitupia mabao 11 kwenye mechi  11 alizocheza kwa msimu huu kwenye mashindano yote.


SOMA NA HII  FAMILIA YA MARADONA YAANZA KUVURUGANA KISA MALI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here