Home Uncategorized HESABU ZA SIMBA NI KWA WANIGERIA, SVEN ATOA NENO

HESABU ZA SIMBA NI KWA WANIGERIA, SVEN ATOA NENO


 BAADA ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba kuweka rekodi yao ndani ya msimu wa 2020/21 kwa kupata ushindi wa mabao mengi bila kufungwa kwenye mchezo mmoja hesabu zao kwa sasa ni kwenye mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika.


Simba iliifunga Coastal Union mabao 7-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha ikiwa ni rekodi ya mabao mengi kupatikana ndani ya dakika 90 kwa msimu wa 2020/21.


Timu ya kwanza kufunga mabao mengi kwa msimu huu kwenye mchezo mmoja ilikuwa ni JKT Tanzania, ambapo iliifunga Mwadui FC mabao 6-1 Uwanja wa Mwadui Complex na hat trick ya kwanza ilipatikana kupitia kwa Adam Adam ambaye amefunga jumla ya mabao sita.

 Kwenye mchezo huo uliochezwa Novemba 21, John Bocco nahodha wa Simba naye alifunga hat trick ya kwanza kwa Simba ikiwa ni ya pili ndani ya ligi.

Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa kwa ushindi ambao wameupata inawapa picha ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa awali dhidi ya Plateua United ya Nigeria licha ya kwamba haitakuwa kazi nyepesi.


“Ushindi mbele ya Coastal Union ni furaha kwetu na unatupa picha ya kile ambacho tunakihitaji ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika licha ya kwamba sio kazi nyepesi.


“Kila mchezaji ameonekana kufurahi na inaleta matumaini kwamba tutakwenda kupambana ili kufanya vizuri, malengo yetu ni kuona kwamba tunapata ushindi,” amesema.

Kikosi cha Simba kinatarajiwa kutimka Bongo Jumatano kuelekea Nigeria kwa ajili ya kujiweka sawa kwa mchezo wa awali unaotarajiwa kuchezwa kati ya Novemba 27-29.

SOMA NA HII  HAYA HAPA MAJUKUMU YA SENZO NDANI YA YANGA, KIBALI CHAKE BADO KIPO SIMBA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here