Home Uncategorized ISHU YA SIMBA KUYUMBA MSIMU WA 2020/21, SIMBA YAFAFANUA

ISHU YA SIMBA KUYUMBA MSIMU WA 2020/21, SIMBA YAFAFANUA


 UONGOZI wa Simba umesema kuwa kwa sasa unaamini kwamba una nguvu ya kutetea taji la Ligi Kuu Bara kwa mara nyingine tena licha ya kuanza kwa kuyumba ndani ya msimu wa 2020/21.


Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kwenye maisha ya soka kuna mapito ya kipekee ambayo wakati mwingine unashindwa kuwa na chaguo kutokana na matokeo ambayo unayapata jambo ambalo linasababisha timu kuyumba kiasi chake.


Kwenye mechi mbili mfululizo zilizopita Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck ilikuwa kwenye wakati mgumu baada ya kuyeyusha pointi sita jumlajumla ndani ya uwanja.


Hali hiyo ilipelekea kufanya mabadiliko kwenye benchi la ufundi kwa kumtimua kocha wa makipa Muharami pamoja na aliyekuwa meneja wa timu hiyo kwa wakati hu Patrick Rweyemamu.

Ilifungwa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons na ilinyooshwa ba 1-0 dhidi ya Ruvu Shoting jambo ambalo liliwapa maumivu mashabiki wa Simba pamoja na viongozi kiujumla.


Manara amesema:”Kwenye maisha ya soka kuna matokeo magumu na ya ajabu wakati mwingine ndivyo ambavyo soka lipo lakini hakuna sababu ya kukata tamaa kwa sababu ni nyakati ambazo tunapitia.


“Bado imani yangu ni kwamba kikosi chetu ni imara na tunaweza kutetea taji letu tena kwa msimu wa 2020/21 hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti.”


Simba ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi 16 baada ya kucheza mechi 8 ndani ya ligi kinara ni Azam FC mwenye pointi 22.

SOMA NA HII  MTIBWA SUGAR KESHO KUMALIZANA NA COASTAL UNION