Home Uncategorized JEMBE LA KAZI YANGA KAMILI GADO KUIVAA AZAM FC, LAANZA MATIZI

JEMBE LA KAZI YANGA KAMILI GADO KUIVAA AZAM FC, LAANZA MATIZI

 


NAHODHA wa Yanga, Lamine Moro, kwa sasa yupo fiti baada ya kupata maumivu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba, Novemba 7.


Moro hakuweze kumaliza dakika 90 kwenye mchezo huo uliokamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

 

Beki huyo alitolewa nje katika kipindi cha pili cha mchezo wa Dar es Salaam Dabi iliyopigwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Mkapa.

 

Katika mchezo huo, Moro alitolewa kwa kubebwa kwenye machela baada ya kugongana na beki wa kulia wa Simba, Shomari Kapombe ambaye yeye aliendelea na mchezo huo.

 

 Meneja Mkuu wa timu hiyo, Hafidh Saleh, amesema kuwa beki huyo hajapata majeraha makubwa baada ya jopo la madaktari, linaloongozwa na Shecky Mngazija, kumfanyia vipimo vya X-Ray.

 

Saleh amesema kuwa baada ya kuonekana majeraha hayakuwa ya kiwango kikubwa, beki huyo alianza mazoezi mepesi ya binafsi huku akiendelea na matibabu katika kujiandaa na michezo ijayo dhidi ya Namungo FC na Azam FC.

 

“Lamine tulimfanyia vipimo na majibu yalionyesha kuwa hakukuwa na hatari yoyote kubwa kwenye goti lake, ulikuwa ni mgongano wa kawaida kati yake na Kapombe.

 

“Ingawa mgongano huo ulimsababishia maumivu makali hapo kabla lakini baada ya vipimo vya X-ray, tumempatia dawa na sasa yuko tayari kuanza mazoezi taratibu.

 

“Hivyo, upo uwezekano mkubwa wa kuwepo sehemu ya kikosi kitakachocheza michezo yetu miwili ya ligi dhidi ya Namungo kabla ya kucheza na Azam,” amesema Saleh.

SOMA NA HII  MIKONO YA DHAHABU YA ABAROLA YAPOTEZWA NA MANULA