Home Uncategorized KAGERE HATIHATI KUIKOSA YANGA NOVEMBA 7, ISHU YA MUGALU IPO HIVI

KAGERE HATIHATI KUIKOSA YANGA NOVEMBA 7, ISHU YA MUGALU IPO HIVI


  

MSHAMBULIAJI namba moja wa Klabu ya Simba kunahatihati akaikosa Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Novemba 7 Uwanja wa Mkapa.


Kagere ametupia jumla ya mabao manne ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa nyuma ya kinara wa Azam FC ambaye ni Prince Dube mwenye mabao sita.


Nyota huyo aliumia kwenye mchezo wa ligi dhidi ya JKT Tanzania wakati waliposhinda kwa mabao 4-0 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.


Kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa mshambuliaji wake Kagere bado ana majeraha anaweza kurejea uwanjani baada ya wiki mbili kumeguka.


“Kagere ana majeraha ya muda mrefu lakini anaweza kurudi baada ya wiki mbili au tatu mbele ndani ya uwanja.


“Kuhusu hali ya Chris Mugalu muda wowote naye anaweza kurejea kwenye ubora wake ili kuiongoza safu ya ushambuliaji,” amesema.


Mugalu jana Novemba 4 alianzia benchi wakati Simba ikishinda mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Uhuru.


Alipata muda wa kuingia pia dakika ya 63 akichukua nafasi ya nahodha John Bocco ambaye alitupia bao moja.

SOMA NA HII  KIFAA MAALUMU CHA MORRISON MAZOEZINI CHAIBUA GUMZO