Home Uncategorized MO DEWJI AWATULIZA SIMBA, AWAAMBIA CHAMA ANA MKATABA MREFU SIMBA

MO DEWJI AWATULIZA SIMBA, AWAAMBIA CHAMA ANA MKATABA MREFU SIMBA




Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mohamed Dewji amesema klabu hiyo ilishaingia mkataba mpya na kiungo Cleotus Chama.


Mo Dewji amesema mkataba wao na Chama unaisha mwaka 2022, hivyo taarifa za kuwa anakwenda Yanga zimekuwa zikiwashangaza.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Dewji amesema mchezaji huyo ni mali ya Simba na hakuna sababu ya kuwa na hofu.


“Taarifa sijui anakwenda Yanga ni mambo ambayo si sahihi, hakuna sababu ya kuwa na hofu na ninawatoa hofu mashabiki wa Simba kuwa tuko makini sana.


“Sehemu mbalimbali zimekuwa nikikutana na mashabiki wa Simba ambao wananiambia Mo fanya Chama asiondoke Simba. Chama ni mchezaji wa Simba.


“Suala kwamba anakwenda Yanga sijui linatoka wapi lakini haina shida, sasa nimewaambia na ninafikiri leo tunafunga mjadala,” alisema Mo Dewji.


SOMA NA HII  SIMBA: LAZIMA TUTUSUE KIMATAIFA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here