Home Uncategorized MO DEWJI: SIMBA HAINA HELA

MO DEWJI: SIMBA HAINA HELA


MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Klabu ya Simba, Mohamed Dewji amesema kuwa hela zote za usajili yeye anatoa kwa kuwa timu hiyo haina hela.

Jana, Novemba 15 Dewji alizungumza na Waandishi wa Habari na kuweka bayana mpango wa timu hiyo ni kufika mbali kimataifa.

Dewji ameweka wazi kuwa miongoni mwa wachezaji ambao ametoa pesa zake na kuwasajili ni pamoja na kiungo mshambuliaji Luis Miquissone pamoja Clatous Chama.

Suala la Chama lilivuta hisia za wengi ambapo habari zilikuwa zinaeleza kuwa yupo kwenye rada za Yanga jambo ambalo ameliweka wazi kwa kusema kuwa nyota huyo ana mkataba na Simba mpaka 2022.

Dewji amesema:-“Bado hatujaandaa bajeti ya usajili, hivi sasa tunasubiria mapendekezo ya wachezaji ambao kocha anawahitaji, lakini Simba haina hela ila mimi ndio natoa hela.


“Katika hilo la usajili nimepanga kuja na utaratibu mpya wa usajili wa wachezaji wetu kwa kuwapa mikataba mirefu kwa kuanzia miaka minne kwenda mbele,” amesema.

SOMA NA HII  KUNA JAMBO HUKO JANGWANI KESHO NDANI YA CHAMPIONI JUMAMOSI